CHUO CHA MIPANGO DODOMA CHAIBUKA KIDEDEA MASHINDANO YA MICHEZO YALIYOFANYIKA MJINI MOSHI MKOANI KILIMANJARO

 Katika picha ni uongozi wa chuo cha Mipango Dodoma, wakiwa katika hafla fupi ya kuwapongeza wachezaji waliowakilisha chuo hicho huko Mjini Moshi, baada ya kurejea na ushindi.

Na mwandishi wetu 
Mkuu wa chuo cha Mipango ya maendeleo vijijini mkoani Dodoma Mheshimiwa Mayaya, amepongeza ushidi wa kishindo katika mashindano ya michezo mbalimbali yaliyofanyika  hivi karibuni huko mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, yakihusisha takribani vyuo 15.
Akizungumza na wanamichezo hao katika hafla fupi ya kuwapongeza wanamichezo hao, ameoonesha kufurahishwa na jitihada za wanamichezo hao walioiletea heshima taasisi hiyo na hivyo kuahidi kutoa ushirikiano wa dhati katika suala la michezo chuoni hapo.
Katika mashindano hayo Chuo cha mipango kimejishindia medali 20 katika mchezo wa riadha ambapo mshindi wa kwanza ,pili na tatu wote wametoka katika chuo hicho. Michezo mingine iliyowapatia ushind i ni mpira wa miguu ambapo timu y chuo cha mipango iliweza kuwapiga goli 2-0 TIA ya Dar es Salaamu huku akiipiga IFM Vikapu 66 kwa 63 katika mipra wa kikapu.
Katika mchezo wa riadha Bwana Hamphley Makava aliweza kushika nafasi ya pili katika mbio za meta 100 akitumia sekunde 11 na pointi 51 huku akizidiwa na mshindani mwenza kwa pointi 3 ndugu Twalib aliyetumia sekunde 11 na pointi 48 na kuibuka mshindi wa kwanza.

Comments