Mtu aliyezua gumzo hivi karibuni kwa kujiita nabii Tito, ambaye jina
lake halisi ni Onesmo Machija, mwenye umri wa miaka 44 amepelekwa
hospitali ya Mirembe Dodoma kwa ajili ya matibabu ya akili.
Hii ni baada ya kubainika kuwa mtu huyo ana matatizo ya akili kupita mahojiano baina yake na jeshi la polisi mkoani Dodoma.
Hayo yamebainishwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma Gillesi Muroto wakati akizungumza na wanahabari.
Kamanda Muroto amefafanua
kuwa, mnamo tarehe 23 Juni 2014 mtu huyo alilazwa hosipitali ya taifa
ya muhimbili kwaajili ya matibabu ya akili, ambapokwa mujibu wa taarifa
za kidaktari alipaswa kurejea hosipitalini hapo tarehe 9 mwezi Julai
mwaka huohuo lakini hakurejea, na matokeo yake hivi karibuni aliibuka
katika kijiji cha Nghong'ona kilichopo jirani na chuo kikuu cha Dodoma
(UDOM) na kuendesha mahubiri ya kidini yasiyozingatia maadili huku
kanisa lake likiwa halitambuliki.
Kufuatia hali hiyo Jeshi la polisi
lilimshikilia na kufanya mahojiano naye na ndipo ilipobainika kuwa mtu huyo ana matatizo yaakili na hatimaye alifikishwa katika
hosipitali ya rufaa ya Mirembe iliyoko mjini Dodoma kwaajili ya
uchunguzi ambapo Daktari Dixon Philipo baada ya kumfanyia vipimo alitoa
uthibitisho kuwa mtu huyo bado ana matatizo ya akili.
Comments