Je,unajua siri ya wanasiasa wa vyama vya upinzani kuhama vyama vyao na kukimbilia chama Tawala?
Hivi karibuni kumezuka wimbi kubwa la wanachama wa vyama vya upinzani kuvihama vyama vyao na kukimbilia chama tawala CCM. Hata hivyo licha ya wao kueleza sababu za kuhamia Cha ma hicho, bado umekuwepo mshangao miongoni mwa wanajamii katika kutathmini namna wanasiasa hao machachali wanavyohama. Siri kubwa inayowafanya kuhamia cha ma hicho ni kuridhishwa na utendani mzuri wa cha ma tawala CCM katika kusimamia raslimali za taifa. Ikumbukwe kuwa lengo la cha ma chochote siyo kuharibu Bali ni kujenga, na hivyo kuleta maendeleo ya pamoja. Utakumbuka kuwa kipindi cha nyuma CCM iliwahi kuendesha kampeni ya kujivua gamba hasa baada ya kukithiri kwa tuhuma za utendaji mbovu miongoni mwa wanachama wake. Huo ni ujasili mkubwa kwa chama kujitathmini na kuchukua hatua za kujisahihisha jambo ambalo ni msingi wa kuigwa kwa vyama vingine. Hadi sasa matuda ya mikakati ya CCM yanaonekana na mojawapo ni kuvuna wanachama wapya wakiwemo wa upinzani. Hata hivyo pamoja na kuwepo muungano kati ya vyama vya upinzani na chama tawala usitafsiliwe kama ni viashiria vya kuzorota kwa upinzani nchini. Katika ulimwengu wa sasa umuhimu wa vyama vya upinzani bado ni mkubwa sana hasa katika nchi zinazoendelea, kwani ndiyo silaha ya pekee katika kuinua demokrasia na msingi wa kupima utendaji wa serikali.
Ni ukweli usiopingika kuwa Hali ya kukithiri kwa rushwa na ufisadi sasa imepungua sana kama siyo kuisha kabisa,na imani ya wananchi dhidi ya serikali na viongozi wake inaongezeka kila uchao. Kwa upande mwingine vyama vya upinzani hususani Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na CUF wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha Uhuru wa wananchi kisiasa kiuchumi na kijamii, jambo ambalo ni faida ya jamii mzima.
Wito wangu kwa wadau wote wa siasa ni kwamba waendelee kuishi kwa kuheshimiana na kuthaminiana kama ilivyo desturi ya watanzania, tusahau tofauti zetu na kuishi kama ndugu. Hii ni kwa sababu jitihada za serikali sasa zinaonekana hivyo ikiwa kweli tunahitaji maendeleo ni lazima sasa tuwe na sauti moja.
Comments