Na Stephen Jackson
Shangwe imegubika viwanja vya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Kufuatia ushidi wa timu ya mpira wa miguu ya chuo kikuu cha Zanziba, kuitandika magoli 4 kwa 2 timu ya chuo kikuu cha Mtakatifu John ali maarufu ST. John cha Dodoma katika mchezo wa fainali za shirikisho la michezo vyuo vikuu Tanzania (TUSA) lililohusisha vyuo mbalimbali vya Tanzania.
Mashindano hayo yalizinduliwa rasmi na waziri wa habari,
sanaa,utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe mnamo Desemba 14 katika viwanja vya chuo kikuu cha Dodoma na kuhitimishwa na Naibu waziri wa habari,Juliana Shonza, ambapo timu ya chuo kikuu cha Zanzibar imeibuka kidedea. Aidha katika hotuba yake Naibu waziri Shonza ameviasa vyuo husika kutoa ushirikiano katika mashindano mbalimbali.
Comments