ASKOFU WA JIMBO KUU KATHOLIKI LA DODOMA BEATUS KINYAIYA AMEWATAKA VIJANA KUJIAJIRI


Na Stephen Jackson

Ikiwa ni katika kuadhimisha sikukuu ya mwaka mpya 2018 katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma,Mhashamu askofu wa jimbo katoliki la Dodoma Beatus Kinyaiya ametumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuachana na manung'uniko ya ukosefu wa Ajira kwani kufanya hivyo ni kushindwa kuchangamkia fursa zilizopo.
Mhashamu Askofu Kinyaiya amesema hayo  tarehe moja januari 2018 katika parokia ya Chamwino Ikulu,wakati akiendesha ibada ya kipaimara. Aidha amewasisitiza vijana kuachana na manung'uniko ya ukosefu wa Ajira na badala yake watumie fursa ya uwepo wa makao makuu ya nchi katika mji Wa Dodoma kama fursa ya pekee ya kujiletea maendeleo. Aidha amewashauri vijana mkoani Dodoma kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya ufugaji kuku na mingine kadha wa kadha.Pia ametumia fursa hiyo kuwataka waumini kuacha tabia ya umbea kwani haina faida kwa wakristo na maendeleo ya nchi.Katika ibada hiyo jumla watu 94 wamepata kipaimara na kuwa askari kamili wa yesu na wamekabidhiwa jukumu la kuamsha walegevu katika jamii inayowazunguka,na kuwaleta kwa Mungu.

Comments