KWAYA YA UVUKE KUTOKA KANISA KUU LA ANGLIKANA DODOMA YATOA FARAJA KATIKA MSIBA WA MAREHEMU ASHERI DOBOGO HUKO MUNDEMU
Waimbaji wa kwaya ya Uvuke kutoka kanisa kuu la Anglikana Dodoma,wametoa faraja katika msiba wa Mwalimu mstaafu Marehemu Asheri D. Dobogo aliyefariki siku ya Alhamisi tarehe 18/01/2018 nyumbani kwake kijijini Mundemu wilaya ya Bahi baada ya kuugua.
Katika msiba huo watu wengi wamejitokeza kutoa faraja nyumbani kwa marehemu ikiwemo kwaya ya Uvuke ambayo kimsingi ilionesha mfano mzuri wa kuigwa kutokana na uimbaji wao wa kupiga mziki wa taratibu na nyimbo zenye kutia moyo wakati wote.
Pamoja na hayo pia kulikuwa na waimbaji wenyeji ambao kwa pamoja walilifanya tukio hilo kuwa lenye kugusa hisia za watu.
Kwaya hiyo ilifika katika msiba huu kufuatia mwanakwaya mwenzao Heriet Dobogo kufiwa na baba yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa kwaya hiyo kushirikiana katika shida na raha pindi mmoja wao anapofikwa na jambo linalogusa jamii. Marehemu Asheri Dobogo atazikwa siku ya jumapili tarehe 21/01/2018 nyumbani kwake kutokana na wasia aliouacha. Bwana alitoa bwana ametwaa Jina la Mungu lihimidiwe.
Comments