WEMA SEPETU AKASIRISHWA NA MANENO YA MKE WA NABII TITO, AJIANDAA KUMBURUZA MAHAKAMANI KWA KUMDHALILISHA.

Msanii mahili wa filamu za kitanzania (Bongo movie) Wema  Isack Sepetu amevunja ukimya kufuatia kauli za mke wa nabii Tito alizosisambaza mitandaoni akimshawishi msanii Wema aolewe na nabii huyo.Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii, msanii huyo alikiri kuziona video hizo na kudai kuwa zimemkasirisha sana.''Kiukweli wameniudhi sana kwa kunidhalilisha, nawasiliana na mwanasheria wangu ili nimburuze mahakamani mwanamke huyo" alisema Wema.

Ikumbukwe kuwa jeshi la polisi mkoani Dodoma lilimkamata  nabii Tito ambaye baada ya mahojiano alibainika kuwa na matatizo ya akili na kupelekwa hosipitali ya Mirembe kwa matibabu.
Kwa mujibu wa jeshi hilo jitihada za kuwatafuta mke na mjakazi wa nabii huyo zinaendelea, ambapo kamanda wa polisi mkoa Dodoma Gillesi Muroto alidai bado wanashauriana juu ya hatua za kuchukua dhidi ya mtuhumiwa ndugu Onesmo Machibya.

Comments