HALMASHAURI YA CHAMWINO YAFANIKISHA UZINDUZI WA MPANGO MAALUMU WA KUSHIRIKISHA WADAU KUCHANGIA ELIMU.
Katika picha ni mheshimiwa diwani wa kata ya Buigiri (aliyesimama)akitolea ufafanuzi taarifa ya wadau waliochangia elimu katika kuinua kiwango cha ufaulu.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, imeanza kutekeleza mpango maalumu wa kuinua ufaulu wa wanafunzi katika matokeo ya mitihani ya taifa kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa elimu.
Waziri wa nchi, Tawala za mikoa na serikali za mitaa Seleman Jafo (kulia kwako) akiwa na viongozi wa wilaya ya Chamwino, wakijiandaa kukabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi wenye uhitaji.
Akitolea ufafanuzi taarifa ya wadau waliochangia vifaa vya Elimu tarehe 7 Februari 2018, diwani wa kata ya Buigiri mheshimiwa Kenneth Edward Yindi alibainisha kuwa Wilaya hiyo imekuwa ikifanya vibaya kwa miaka miwili mfululizo katika ngazi ya mkoa na taifa.
“Kwa kipindi cha miaka miwili sasa matokeo ya mitihani ni mabaya sana, mfano mwaka huu 2018 tumekuwa ni Wilaya ya saba kati ya wilaya nane kimatokeo kimkoa hii ni ishara mbaya kwani tutashindwa kushiriki kikamilifu kwenye Tanzania ya viwanda” Alisema Yindi.
Mheshimiwa Yindi ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa halmashauri hiyo kufanya jitihada za pekee katika kuikomboa wilaya hiyo dhidi ya matokeo yasiyoridhisha. “Kupitia hadhara hii kwa niaba ya Kata ya Buigiri niwanawomba mkurugenzi wa Halmashauri na watalaamu wake katika idara ya Elimu watutoe katika hili janga la matokeo mabaya” Aliongeza Yindi.
Kufuatia hali hiyo halmashauri ya wilaya ya Chamwino kwa kushirikiana na diwani huyo na Wahadhili wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Dr.Ombeni Msuya na Dr. Abdalah Seni ambapo kwa kuzingatia waraka wa Elimu no.6 mwaka 2015 kipengele cha 3.7 kinachoruhusu wadau kushiriki katika uchangiaji elimu, tayari wameanzisha utaratibu maalumu wa kuchangia vifaa vya shule kwa wanafunzi wenye uhitaji maalumu.
Mpango huo umezinduliwa rasmi na Waziri wa Nchi, Tawala za mikoa na serikali za mitaa mheshimiwa Seleman Jafo (Mb) ambapo Jumla ya daftari 8550
zilikuwa zimepatikana kutokana na michango ya wadau wa elimu mkoani Dodoma.Vifaa vingine vilivyopatikana ni pamoja na penseli,vifutio na vichongeo.
zilikuwa zimepatikana kutokana na michango ya wadau wa elimu mkoani Dodoma.Vifaa vingine vilivyopatikana ni pamoja na penseli,vifutio na vichongeo.
Mpango huo ulizinduliwa kitaifa katika shule ya msingi Uguzi iliyopo kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma na unajulikana kwa kauli mbiu isemayo “Nisaidie peni na daftari nami nipate Elimu”
Aidha mpango huo unalenga kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli za kutoa elimu bila malipo kwa kutumia utaratibu maalumu wa uchangiaji utakaosaidia kuondoa mianya ya baadhi ya walimu kujinufaisha na michango holela iliyopigwa marufuku na serikali.
Miongoni mwa wadau waliochangia ni pamoja na:
- EFFCO SOLUTION TANZANIA,NIPO GROUP DODOMA, KIWANGO SECURITY, GLOBAL COMPANY LTD, BRIG. M. MNDEME, KENNETH GONDWE, MH. ASIA HALAMGA, KATIBU UVCC (MK) DODOMA, MH.DEO NDEJEMBI, DKT. OMBENI MSUYA, DKT ABDALLAH J SENI, ROSEMARY KENNETH YINDI, KIJIJI CHA MWEGAMILE, KIJIJI CHA CHINAGALI 2, KIJIJI CHA BUIGIRI, PROF. SIZA TUMBO, MH. L.LUSINDE (MB), MH .J. MWAKA MAKANYAGA (MB), FARIDA MGOMI, Mwenyekiti UWT-PWANI, na ndugu RAMADHANI HASSANI, mwandishi wa gazeti la MTANZANIA.
Serikali imetoa shukrani kwa wadau hao na kuwaomba wasivunjike moyo katika kufanikisha maendeleo ya elimu nchini.
Comments