Na Stephen Jackson
Mpendwa msomaji, asante kwa kutembelea blog yako makini, ambayo kimsingi lengo lake ni kushirikiana nawe katika kuyafikia mafanikio.
Mada ya leo je, unafahamu kuwa mafanikio ya mtu huanza na kujiamini? Neno kujiamini limezoeleka sana masikioni mwa kila mtu na ni miongoni mwa maneno yanayotumiwa kila siku.
Kujiamini ni ile hali ya kujikubali kuwa wewe unao uwezo wa kufanya kitu fulani kwa ubora sahihi pasipo shaka yoyote.
Kiujumla kila jambo analolitenda mtu ni matokeo ya kujiamini kwake ambapo ndipo humpeleka kwenye mafanikio ya jambo analolifanya. Wengi huwa tunasafiri mara kwa mara kutokana na harakati za kimaisha. Dereva ndiye hupanga safari yake na kuisimamia kikamilifu hadi mahali anapokwenda.Hivyo ikitokea amefanya kosa lolote katika kudhibiti chombo chake cha usafiri, anaweza kusababisha ajali ambayo kimsingi haitamuathiri peke yake ni lazima abiria pia watapata madhara. Hivyo mafanikio ya safari yanatengemea jinsi gani dereva anajiamini.Katika maisha yako wewe ndiye dereva na wengine wote ni abiria wako hivyo ni lazima ujiamini kwanza ndipo watu wakuamini juu ya kila jambo unalopanga kufanya. Hebu tuchungulie mifano michache tu ya mambo ambayo mtu asipojiamini anaweza asifikie malengo.
KUFANIKIWA KIBIASHARA:- Ili mtu afanikiwe katika biashara yake,ni lazima ajiamini katika mambo yafuatayo; Kwanza aamini kuwa anao uwezo wa kufanya biashara, anao muda wa kutosha kufanya biashara, anao washauri sahihi kuhusu biashara yake, bidhaa zake ni za muhimu sana kwa wateja wake, na mazingira ya biashara yake ni salama kwake na wateja wake pia.
Hivyo ikiwa unafanya biashara kwa kuuza bei ambayo hata wewe unaamini usingepeda kuuziwa, au bidhaa yako ni bandia na haifaikwa matumizi yako basi usitegemee mafanikio yoyote. Mathalani siku hizi kumekuwa na mtangazo mengi ya waganga wa jadi juu ya bidhaa zao zinazodaiwa kusheheni uwezo wa kubadilisha maisha ya watu katika nyanja mbalimbali.Je ukweli upo kwa kiasi gani? Nini mafanikio yao dhidi ya matumizi ya bidhaa hizo? Je wao wenyewe wanazitumia? Jiamini kuwa jitihada zako binafsi katika biashara yako ndiyo njia pekee ya kuzifikia ndoto zako na ujiepushe na maneno ya upotoshwaji.
KUPATA MCHUMBA / MWENZI BORA: Vijana wengi wa kike na kiume mara nyingi hupenda kuwa na mahusiano na wenza wenye sifa nzuri na za kuvutia. Wadada wenye maumbile mazuri ya kuvutia wamekuwa wakiteka soko la mahusiano huku wale wenye mapungufu wakibaki na upweke na wengine wakijuta kuzaliwa. Upo ushahidi wa kutosha kuwa uzuri wa mtu ni tabia njema. Ukijenga moyo wa kujiamini na kuishi katika misingi ya tabia njema ni lazima kasoro zako za kimaumbile zitafichwa na tabia na mwenendo wako. Wasichana wengi na wanawake wanaohisi kuwa wana kasoro katika maumbile yao wamekuwa wakijaribu kujisahihisha kasoro hizo kwa kujipamba kupita kiasi mfano kujichubua na kuvaa nguo angavu zinazowachora maumbile yao na zinazo wabana, jambo ambalo huwafanya baadhi yao kuwa viumbe wa kutisha badala ya kuwa na mvuto. Siku hizi Mathalani, huwezi kumkuta kijana wa kiume au wa kike akitamba na mwenza mwenye mapungufu ya wazi kama vile ulemavu wa viungo, kasoro za maumbile au sura isiyo na mvuto. Pia hata katika tabia na mienendo ni vilevile, hakuna anayependa kuwa na mwenzi mwenye tabia au mwenendo mbaya. Lakini kama umewahi kuchunguza utagundua kuwa wengi wenye tabia na mienendo mibaya ndio hawana uvumilivu kwa wapenzi wao. Hivyo ili kupata mwenzi bora ni lazima ujiamini kuwa wewe ni bora sana kiasi kwamba unahitaji mtu wa aina yako mwenye taabia na mwenendo mwema kama wako. Kwa wanandoa pia msitegemee miujiza kama tabia zinapishana. Ni lazima wote mlingane tabia ndipo upendo wenu utadumu. Akina dada ni lazima mshituke kuwa uzuri haupatikani dukani, ni lazima uzuri wako utoke moyoni mwako kupitia tabia na mwenendo mwema. Vinginevyo matarajio yenu yatakuwa hayafiki kwa wakati. Kila mtu anapaswa kujikubali vile alivyo kuwa anastahili na anafaa katika jamii. Akina kaka wengi mnapochagua wachumba msiwe na tamaa ya maumbile, zingatieni mafundisho ya dini zenu na maadili halisi ya jamii mnazoishi. Msitekwe na tamaduni za kigeni zinazoletwa na utandawazi. Daima mafanikio yanakutaka ujenge tabia ya kuamini kile kilichopo ndani yako na ukisimamie kikamilifu.
KUMILIKI MALI NYINGI: Wengi wanaomiliki mali nyingi tumezoea kuwaita matajiri. Hawa ni watu wenye malengo na mikakati mikubwa katika jitihada zao za kila siku.Ni watu wanao jiamini sana katika matumizi ya rasilimali zao, wana mipangilio madhubuti na kumbukumbu zote muhimu zinazohusu matukio mbalimbali na fursa za kiuchumi. Ikiwa unapenda kumiliki mali nyingi ni lazima ujiamini kuwa unao uwezo na sifa zinazoendana. Matajiri wengi ni wafanya biashara wakubwa.
Hivyo kabla hujafikiria kuwa tajiri ni lazima kwanza ufikirie kuwa mfanya biashara mkubwa na kabla hujafikiria kuwa mfanya biashara mkubwa ni lazima uanze kuwa mjasiria mali wa kawaida na ndipo uanze kupanda daraja katika kuyafikia mafanikio. Bila kujiamini huwezi kuaminiwa na mtu yeyote hivyo nafasi yako ya mafanikio inatokana na jinsi unavyojiamini.Jiulize ni kitu gani ambacho una uwezo mkubwa wa kukisimamia na kikazaa matunda? hicho ndicho unaweza kuanza nacho kama mjasilia mali na hatimaye kitakua na kufikia hatua kubwa ya mafanikio. Mfano mzuri ni ubunifu wa msanii maarufu wa mziki wa bongo fleva Nasibu Abdul maarufu kwa jina la "Diamond" aliangalia uwezo wake aliokuwa nao wa kuuza karanga akaamua kuuboresha. Matokeo yake siku hizi vijana wengi waliokuwa wakiona aibu kuuza karanga na walikuwa pengine wakijificha wasionwe na wapenzi wao, na hata jamaa zao lakini kupitia jitihada za Diamond sasa uuzaji karanga umekuwa ni fasheni na vijana wengi wamejiingiza kwenye biashara hiyo na matokeo yake mahitaji ya uzalishaji karanga yanaweza kuongezeka na hivyo kuinua pato la wakulima wa karanga nchini. Kumbuka ikiwa unachokifanya huna uwezo nacho, fahamu kuwa kamwe hakiwezi kukupa afanikio.Hivyo ili ufanikiwe ni lazima ujiamini kuwa unafahamu unachokifanya.
Hivyo kabla hujafikiria kuwa tajiri ni lazima kwanza ufikirie kuwa mfanya biashara mkubwa na kabla hujafikiria kuwa mfanya biashara mkubwa ni lazima uanze kuwa mjasiria mali wa kawaida na ndipo uanze kupanda daraja katika kuyafikia mafanikio. Bila kujiamini huwezi kuaminiwa na mtu yeyote hivyo nafasi yako ya mafanikio inatokana na jinsi unavyojiamini.Jiulize ni kitu gani ambacho una uwezo mkubwa wa kukisimamia na kikazaa matunda? hicho ndicho unaweza kuanza nacho kama mjasilia mali na hatimaye kitakua na kufikia hatua kubwa ya mafanikio. Mfano mzuri ni ubunifu wa msanii maarufu wa mziki wa bongo fleva Nasibu Abdul maarufu kwa jina la "Diamond" aliangalia uwezo wake aliokuwa nao wa kuuza karanga akaamua kuuboresha. Matokeo yake siku hizi vijana wengi waliokuwa wakiona aibu kuuza karanga na walikuwa pengine wakijificha wasionwe na wapenzi wao, na hata jamaa zao lakini kupitia jitihada za Diamond sasa uuzaji karanga umekuwa ni fasheni na vijana wengi wamejiingiza kwenye biashara hiyo na matokeo yake mahitaji ya uzalishaji karanga yanaweza kuongezeka na hivyo kuinua pato la wakulima wa karanga nchini. Kumbuka ikiwa unachokifanya huna uwezo nacho, fahamu kuwa kamwe hakiwezi kukupa afanikio.Hivyo ili ufanikiwe ni lazima ujiamini kuwa unafahamu unachokifanya.
KUONGOZA WATU: Katika mambo yote kuongoza watu ndilo jambo gumu sana ambalo linahitaji ujuzi wa aina mbalimbali. Mtu yeyote anayesimamia shughuli za kibinadamu ni lazima ajiamini sana kuwa yeye anao uwezo mkubwa wa kufanya vizuri kwenye hayo mambo anayo yasimamia. Haiwezekani mtu asiyejua kitu fulani akawasimamia watu wengine wakifanye kwa kuwa hataweza kutathimini matokeo sanifu ya kitu hicho. Ikiwa unahitaji kuongoza watu fulani katika jambo fulani yakupasa uhakikishe unayo maarifa ya kutosha kuhusu jambo hilo kuliko wale unaotarajia kuwaongoza. Mfano zamani wanasiasa wengi alikuwa wanaomba kuwaongoza watu kwa kujinadi kuwa watawafanyia mambo mengi mazuri watu wao bila kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu vyanzo vya rasilimali na sera za nchi. Matokeo yake wakajishushia heshima kwa kuonekana waongo kumbe dhamila zao hazikuwa mbaya. Kwa sasa wanasiasa wengi wanajitahidi kuwa na uelewa mpana kuhusu kile wanachokizungumza ili waweze kukubalika. Hii ni kwa sababu wananchi wengi wamekuwa na uelewa mpana tofauti na hapo awali. Hivyo changamoto nyingi katika usimamizi au uongozi wa watu ni kuwa tajiri wa elimu,maarifa a ujuzi unaokwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Hata kama unayo elimu kiasi gani usije ukajiamini kwamba hakuna mwingine kati ya watu unaowaongoza anayeweza kujua zaidi yako, amini kuwa wapo wanaoelewamambo hata zaidi yako hivyo tengeneza mazingira shirikishi yanayo ruhusu ubunifu wa kila mtu uweze kufanya kazi. Hiyo itakusaidia kupunguza changamoto na kupanua wigo wa ufanisi. Lakini pia msomaji wangu usiwe mtu wa kuongozwa tu maisha yako yote ni lazima fikirie kuwa ongoza wengine katika jambo fulani unaloamini unaweza kufanya vizuri zaidi kuliko wengine. Hiyo itawafanya wengine pia wajifunze kutoka kwako jiamini unaweza.
Comments