SERIKALI IMETOA MSIMAMO KUHUSU WALIOONDOLEWA KAZINI KWA VYETI FEKI NA WASIOKUWA NA VYETI VYA KIDATO CHA NNE.

Serikali imetoa msimamo wake kuhusu sintofahamu iliyokuwepo dhidi ya hatima ya watumishi walioondolewa kazini baada ya uhakiki kutokana na sababu na vigezo vya uhakiki ikiwemo kutokuwa na vyeti vya kidato cha nne nakughushi vyeti.
Kwa mujibu wa serikali Watumishi waliokutwa na kasoro hizo hawana Madai yoyote.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji, Sera Mathias Kabundugulu wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi cha kujadili masuala ya utawala na rasilimali watu kwa mamlaka za serikali za mitaa, wizara na mikoa ambapo amesema watumishi ambao wamebainika na kuondoka wenyewe, wamefutwa kwenye orodha ya watumishi wa umma na hawana madai wanayodai serikalini ukiwa ndio msimamo.

Kabundugulu amesema pamoja na zoezi kukamilika kwa muda ambao umepangwa, wapo baadhi ya maafisa utumishi wameendelea kuwafumbia macho watu wasio kuwa na vyeti vya kidato cha nne.

Comments